Siri Hospitalini

Siri Hospitalini

  • KSh320.00


Jumatatu asubuhi, Malit ameshindwa kuamka ili aende shuleni. Dada yake mdogo, Nashipae, anashangazwa na kulala huku kwake kwa muda mrefu. Je, ni tabia mpya ya Malit ama anaugua? Kwa kawaida, Malit ndiye humwamsha Nashipae kila siku. Nashipae anawaarifu wazazi kisha wanatambua kuwa Malit anaugua. Anapelekwa hospitalini mbiombio. Bi Pulei anapomfikisha mwanawe Malit hospitalini, anagundua kuwa ufisadi umekita mizizi huko. Mama yuko katika njia panda. Atoe hongo ili mwanawe ahudumiwe ama asitoe ili adumishe uzalendo?