KCPE Kiswahili

KCPE Kiswahili

  • KSh621.00
  • Save KSh8


KCPE SCORE MORE KISWAHILI ni kitabu cha marudio kilichoandikwa kwa mujibu wa silabasi kuanzia Darasa la Nne hadi la Nane. Hii ni hidaya adhimu yenye lengo la kumwandaa mwanafunzi wa Darasa la Nane kwa mtihani wa kitaifa. Upekee wa kitabu hiki ni:
• Kinamwelekeza mwanafunzi kuwa na ung'amuzi wa mawanda ya ngeli.
• Weledi wa kutawala safu ya sarufi.
• Msamiati wa kumfanya muanafunzi kuwa mahiri na mwenye kutopea katika matumizi yake.
• Faslu nzima inayomshirikisha katika ufahamu ulio bora.
• Mwongozo wa kuandika insha sheshe pasi na hatihati wala kikweukweu.
• Maswali kila baada ya kipengele yanaitosheleza jazba ya mwanafunzi mrejelewa. - Vielezo vya mtihani wa KCPE vinavyotoa picha halisi ya mtihani wa kitaifa.

Mengi na mengine ni mumu humu kitabui ya kuamsha kani, ari na hamasa ya kuchapuza alama maridhawa. Onja na ufaidi uhondo wa ufanisi.

Waandishi wa kitabu hiki cha marudio ni walimu na watahini wenye tajriba pana ambao wamefudisha katika shule zinazoongoza nchini.


We Also Recommend