Tumaini la Nimara

Tumaini la Nimara

  • KSh379.00


Hadithi zinazofundisha stadi za maisha Hadithi hii ni ya watoto wenye umri wa miaka 12 -14 (Kiwango cha 7-8).
Ni kitabu kinachowasaidia watoto kujifunza na kukuza kujiamini na ujasiri.

Yusufu Miremba ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka kumi na miwili nchini Uganda. Mpango wa wanafunzi kuandikiana barua unaanzishwa baina ya shule yao na nyingine nchini Sri Lanka. Kupitia kwa mpango huo, Yusufu anapiga urafiki na Nimara de Silva kwa njia ya kuandikiana barua. Genge la wanamgambo linamteka nyara Yusufu na kutokomea naye mwituni. Nimara anaanzisha kampeni ya kumwandikia barua kiongozi wa genge hilo pamoja na wengine wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni akiomba Yusufu aachiliwe huru. Haya yote yakiendelea, Yusufu anakula mwata mwituni. Je, kampeni za Nimara zitafua dafu? Je, Yusufu ataachiliwa huru? Watawahi kuonana ana kwa ana?


We Also Recommend