Wimbo Wa Ujasiri

Wimbo Wa Ujasiri

  • KSh379.00


Hadithi zinazofundisha stadi za maisha Hadithi hii ni ya watoto wenye umri wa miaka 12 -14 (Kiwango cha 7-8).
Ni kitabu kinachowasaidia watoto kujifunza na kukuza kujiamini na ujasiri.

Kip Kibet ni mwanafunzi mwenye haya katika shule moja ya upili jijini Nairobi. Wakati wa Tamasha za Muziki katika tarafa ya Nairobi, anagongana na Brenda Njoroge kiajali. Tangu kisa hicho Kip anashindwa kumsahau Brenda. Kip anajiunga katika kwaya ya shule akikusudia kutangamana na Brenda. Mwalimu wake wa muziki anatambua kipawa chake cha kuimba. Anamfanyisha mazoezi ya kina hadi Kip anaibuka kuwa mwimbaji stadi. Hatimaye, Kip anateuliwa kushiriki katika kitengo cha mwimbaji mmoja, wakati wa tamasha za muziki kwenye tarafa. Hata hivyo, anapofika kwenye jukwaa, anasahau wimbo wake. Brenda anamtia moyo akimhimiza kuonyesha ubingwa wake. Je, Kip atafaulu?


We Also Recommend